C

C

Tuesday, April 29, 2014

POLISI NJOMBE YA BANWA NA VIJANA HATARI WA STENDI UNITED



KATIKA kuadhimisha miaka 94 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi nchini mwaka 1919, timu ya polisi Njombe ilishindwa kuonesha cheche zake mbele ya timu ya Stand United ya Njombe baada ya kulazimishwa sare tasa ya bila kufungana.
Timu hizo zilichuana vikali Jumapili iliyopita katika dimba la Sabasaba mjini Njombe katika mchezo ulioshuhudiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani, ukiwa ni mchezo mahususi kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya polisi day.
Hata hivyo mchezo huo ulikosa magori kutoka na kila timu kukosa mbinu za kiufundi kwa ajili ya kuzifumania nyavu licha ya kutengeneza nafasi za kufunga.
Kiongozi wa timu ya Polisi Njombe, Focus Malengo, alisema vijana wake walishindwa kuonesha cheche na kushindwa kufunga kutokana kukosa pumzi kutokana kutofanya mazoezi muda mrefu, kwani waliingia dimbani wakiwa wamefanya mazoezi siku mbili.
“Kwa sasa nitaendeleza mazoezi kwa vijana wangu ili wawe fiti, hapa wanashindwa kufunga kwa sababu hawana mazoezi,” alisema Malengo.
Alisema lengo lililopo sasa ni kuwa na timu ya polisi Njombe itakayokuwa imara na ambayo itafanya vyema katika mashindano mbalimbali nchini.
“Hii timu tukiiendeleza tutakuwa na timu nzuri sana, kwanza mtaji wa wachezaji tunao kabla hatujasajili, wachezaji hawa wakifanya mazoezi vyema halafu tukiongeza na wengine wa kusajili tutakuwa na timu nzuri sana,” alisema.

No comments:

Post a Comment